Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Vyanzo vya usalama vya Iraq vimeripoti kuwa operesheni ya kijeshi ya kulenga magaidi imeanzishwa katika sehemu ya mashariki ya Bonde la Al-Shay, karibu na mji wa Kirkuk.
Operesheni hii imefuatia shambulio la anga la usiku uliopita lililolenga moja ya maficho ya kundi la kigaidi la ISIS katika eneo hilo. Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha usalama, vikosi vya pamoja vimeanzisha operesheni yao moja kwa moja kwenye eneo la tukio. Ripoti za awali zinaonyesha kuwa watu watatu au wanne waliodhaniwa kuwa wanachama wa ISIS wameuawa. Inasemekana kuwa walikuwa sehemu ya seli ya siri (seli fiche) iliyoongozwa na mtu aliyejulikana kwa jina la "Abu Abdulrahman".
Lengo la operesheni hii ni kuchunguza matokeo ya shambulio la anga, pamoja na kusafisha maeneo ya karibu kwa ajili ya kutambua na kuharibu maficho ya chini ya ardhi ya ISIS yanayoweza kuwepo.
Kwa mujibu wa ripoti, huu ni mshambulizi wa tisa wa aina hii mwaka huu dhidi ya maficho ya siri ya ISIS katika eneo la Bonde la Al-Shay. Inafaa kuzingatia kuwa majeshi ya usalama ya Iraq mara kwa mara huendesha operesheni katika maeneo magumu kufikika na ya milimani, ili kukabiliana na mabaki ya magaidi wa ISIS – juhudi ambazo zinatazamwa kama sehemu ya kuhakikisha usalama wa taifa na mapambano dhidi ya ugaidi.
Your Comment